Tarehe 22 Januari, 2020, Balozi Anselm Shigongo Bahati, Balozi wa Tanzania nchini Misri alikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Mohamed Youssef, Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Misri  (Egyptian Businessmen Association) kwa nia ya kukuza na kuimarisha ushirikiano hususan kwenye sekta ya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Misri.