Tarehe 22 Julai, 2020 Mhe. Meja Jenerali (Mst) Anselm Shigongo Bahati, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri alifanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Giza Power kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya pande mbili.

Kampuni hiyo inamiliki kiwanda kikubwa cha kutengeneza nyaya za umeme kwa matumizi mbali mbali. Aidha, Mhe. Balozi alitembelea kiwanda hicho na kujionea uwezo wa uzalishaji wa kiwanda hicho.

Kiwanda cha Giza Power kinafanya biashara ya nyaya za umeme na nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika.