Tarehe 01 Julai, 2020 Mhe. Balozi Anselm Shigongo Bahati,  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mhe. Abdel Fattah Al Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri. Viongozi hao waliahidi kuendeleza ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Misri.