Tarehe 09 Januari 2020, Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati, Balozi wa Tanzania nchini Misri alitembelea Mji wa Viwanda vya Ngozi wa Robbiki  (Robbiki Leather City) nchini Misri na kukutana na uongozi wa Mamlaka wa Robbiki pamoja na kutembelea viwanda vya ngozi mbali mbali vikiwemo kiwanda cha ngozi cha Sarg  (Sarg  Tannery Factory ), kiwanda cha ngozi cha Harby ( Harby Tannery Factory) na kwa nia ya kuwashawishi kuwekeza nchini Tanzania.