Mhe. Meja Jenerali (Mst) Anselm Shigongo Bahati, Balozi wa Tanzania Nchini Misri akipokea rasimu ya Mkataba wa ununuzi wa mahindi ya njano kutoka kwa Mwenyekiti wa kampuni ya Smart Group, Mr. Yasser Attia anaetaka kuingia katika makubaliano ya kibiashara na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makubaliano ya rasimu hiyo yamefanyika katika Ubalozi wa Tanzania nchini Misri,  Jumatatu ya tarehe 30 Novemba, 2020.