Tarehe 16 Januari, 2020, Balozi Anselm Shigongo Bahati alifanya mazungumzo na uongozi wa Chuo Kikuu cha E-JUST kilichopo jijini Alexandira nchini Misri kwa nia ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Misri. Kwa upande wa chuo Kikuu cha E-JUST mazungumzo yaliongozwa na Prof. Ahmed El-Gohary, Rais wa Chuo Kikuu cha E-JUST.