Tarehe 28 Januari, 2020, Mhe. Meja Jenerali Anselm Shigongo Bahati, Balozi wa Tanzania nchini Misri alikutana na kufanya mazungumzo na Kamati ya Baraza la Wawakilishi la Misri linaloshughulikia masuala ya Afrika kwa nia ya kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Misri. Aidha, Mhe. Balozi Bahati na wajumbe wa Kamati hiyo wamezungumzia namna ya kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Misri hususan kwenye masuala ya elimu, utalii, kilimo, ulinzi na usalama kwa maslahi ya pande zote mbili.