Ubalozi wa Tanzania nchini Misri unampongeza kwa dhati Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwa muhula wa pili kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ubalozi pamoja na Diaspora wa Kitanzania waliopo Misri, unaungana na Mhe. Magufuli katika kulitumikia Taifa letu kwa maslahi ya Watanzania wote.