EMBASSY OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA -CAIRO

10, Anas Ibn Malik Street – Mohandessin - Cairo A.R.E

Telephone : (+202) 33374155    -      Fax :  33374286

E-mail: cairo@nje.go.tz

www.eg.tzembassy.go.tz

 

TANGAZO

KUSITISHA HUDUMA ZA KIKONSELI KWA MUDA

Ubalozi wa Tanzania nchini Misri, unapenda kuchukua fursa hii kuwajuulisha kuwa, Huduma za Kikonseli zinazotolewa hapa ubalozini zimesitishwa kwa muda kutokana na tahadhari ya kuenea kwa kasi kwa ugonjwa wa Coronavirus (COVID-19) hadi hapo mtakapotangaziwa baadae.

 Aidha, kwa wale wanaokusudia kuja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuomba pasipoti mpya za kielektroniki, wanaombwa kuahirisha hadi hapo mtakapojuulishwa tena.

 Kwa mahitaji ya Hati ya Dharura ya Kusafiria (ETD), mnatakiwa kufanya maombi kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji, www.immigration.go.tz

UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

CAIRO, MISRI

 

18 Machi, 2020.