Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri unasikitika kutangaza kifo cha Baba Mzazi wa Mhe. Balozi Meja Jenerali (Mst) Anselm Shigongo Bahati kilichotokea leo tarehe 14 Disemba, 2020 majira ya saa 8:00 mchana katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza. Kwa mujibu wa Balozi Bahati, Marehemu atazikwa kijijini kwao Misanga Wilaya ya Kishapu Mkoani Mwanza.

Sote ni wa Mungu na kwake ni marejeo.