Tarehe 06 Januari, 2020, Mhe. Meja Jenerali Anselm Bahati, Balozi wa Tanzania nchini Misri alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Elsayed Waziri wa Kilimo na masuala ya Ardhi wa Misri kwa nia ya kumsalimia na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Misri. Mazungumzo ya viongozi hao yaligusia namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya mifugo, kilimo na uvuvi kati ya nchi hizo mbili.