Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Misri, Meja Jenerali (Mst) Anselm Shigongo Bahati, akifanya mazungumzo na Wamiliki wa Kampuni ya ‘Metal Forming Technology’ wanaokusudia kufanya biashara ya bidhaa za Aluminum nchini Tanzania. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ubalozi wa Tanzania nchini Misri siku ya tarehe 30 Novemba, 2020.

Mhe. Balozi na wafanyabishara hao wamekubaliana kutembelea viwanda vyao vilivyopo katika mji wa Six Oktoba tarehe 05 Disemba, 2020.